DIRISHA LA UDAHILI KWA MUHULA WA MWEZI WA TISA 2022/2023

DIRISHA LA UDAHILI KWA MUHULA WA MWEZI WA TISA 2022/2023

Mkuu wa Chuo DIDES anapenda kuwataarifu kuwa tayari tumefungua dirisha la maombi ya kujiunga na mafunzo ya Astashahada na Stashahada katika fani mbali mbali kwa Mwaka wa Masomo 2022/23 Muhula wa mwezi wa Tisa.

Aidha, Ofisi inapenda kuwataarifu kuwa maombi ya kujiunga yanatakiwa kufanyika kupitia fomu zilizotolewa na chuo. Pia maombi yanaweza kufanyika kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya chuo ya www.dides.ac.tz

Tumeandaa mafunzo malumu kwa wanafunzi watakaojiunga na chuo chetu na kozi fupi zitakazomsaidia mwanafunzi kumjengea uwezo na kupambana na changamoto ya Soko la Ajira.

Nyote mnakaribishwa