DIRISHA LA UDAHILI MWAKA WA MASOMO 2025/2026 KWA MUHULA WA MWEZI WA TATU.

DIRISHA LA UDAHILI MWAKA WA MASOMO 2025/2026 KWA MUHULA WA MWEZI WA TATU.

Mkuu wa Chuo cha Dododma Institute of Development and Entrepreneurship Studies (DIDES) anawataarifu wahitimu wote kuwa dirisha la maombi ya kujiunga na mafunzo ya Astashahada na Stashahada katika kozi ya maendeleo ya jamii (community development) na kilimo (Agriculture Production) kwa mhula wa mwezi wa tatu katika mwaka mpya wa masomo wa  2025/2026 liko wazi.

Aidha, Ofisi inapenda kuwataarifu kuwa maombi yanaweza kufanyika kwa njia mtandao kupitia kwenye tovuti ya Chuo ambayo ni www.dides.ac.tz . Pia maombi yanaweza kufanyika kupitia fomu zetu za maombi zilizoko kwenye tovuti ya chuo na kisha kutumwe kwenye email za Chuo ambazo ni info@dides.ac.tz au didesvet@gmail.com .

Chuo pia kimeandaa mafunzo maalumu yakiwemo ya ujasiriamali yatakayomjengea mwanafunzi uwezo wa kujiajiri na kukabili changamoto mbalimbali wanazoweza kukutana nazo katika soko la ajira kwa wanafunzi watakojiunga na chuo chetu. Wahi sasa nafasi ni chache.

Bonyeza Link hii Kwa maelezo zaidi

Karibu sana

“Mafanikio yako, Malengo Yetu”